Simiyu Jambo Festival yalenga kupiga vita mimba za utotoni

25Jun 2019
Happy Severine
Bariadi
Nipashe
Simiyu Jambo Festival yalenga kupiga vita mimba za utotoni

TAMASHA la Simiyu Jambo Festival linalotarajia kufanyika juni 30 mwaka huu Mkoani Simiyu linakenga kutoa elimu na kupiga vita mimba za utotoni.

wajumbe wa maandalizi ya Simiyu Jambo Festival wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.

Tamasha hilo ambalo ufanyika kila mwaka Mkoani Simiyu limebeba malengo na maudhui ya kuhakikisha linasaidia  kutimiza ndoto za wasichana ambao wanakatishwa masomo kabla ya kuhitimu.

Sambamba na  Tamasha hilo linalofanyika kila mwaka linafanyika kupitia michezo mbalimbali ya asili na kitamafuni ikiwemo mbio za baiskeli kwa wanaume na wanawake, mbio za miguu, mbio za baiskeli kwa walemavu  ,mchezo wa mbina na midahalo .

Akizungumza na waandiahi wa habari ofisini kwake mratibu wa Tamasha hilo Zena Mchujuko amesema  mbali na kutoa elimu pia Tamasha hill limelenga kukuza uchumi wa wasukuma kupitia utamaduni wao.

Zena amesema katika mashindano hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Aksoni Mwansasu na tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi.

Aidha amesema katika tamasha hilo zawadi mbalimbali zenye thamani  ya shilingi mil 32 zitatolewa.

Nae Sanwel Rashid katibu wa chama cha baiskeli Mkoa wa Simiyu amesema katika tamasha hilo kutakuwa na mashindano ya baiskeli ambapo wanaume watakimbia kilomita 150, wanawake kilomita 80 na walemavu kilomita 5 huku mshindi wa kwanza kwa wanaume atapata milioni 1, kwa wanawake 700,000, walemavu 500,000.

Kwa upande wake Mratibu wa Shirika la Idadi ya watu Duniani (UNFPA) mkoani Simiyu Dr. Amir Batenga amesema wanadhamini tamasha hilo kupitia kampeni ya "Wezesha mtoto wa kike apate elimu, atimize ndoto zake" na inawezekana kuzuia mimba katika umri mdogo.

Amesema mabinti wengi wanapata mimba katika umri mdogo hivyo kupitia tamasha hilo litakuwa jukwaa la kufikisha ujumbe kwa jamii ili mtoto wa kike asipate mimba katika umri mdogo.

"Jamii na mtoto wa kike wakielimishwa na kuwezeshwa hawezi kupata mimba katika umri mdogo, tunapoteza mabinti wengi kwa sababu ya kubeba mimba katika umri mdogo...kupitia tamasha hilo tumelenga kuzuia mimba katika umri mdogo ili kuepusha matatizo ya vifo vya uzazi katika umri mdogo" alisema Dr. Batenga

Habari Kubwa