Simulizi aliyemuokoa mtoto kwenye shimo la choo, akipandishwa cheo

23May 2020
Restuta Damian
Bukoba
Nipashe
Simulizi aliyemuokoa mtoto kwenye shimo la choo, akipandishwa cheo

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Maokozi wilayani Ngara mkoani Kagera, ZM3847FC Denis Minja amepandishwa cheo na kuwa ZM 3847 KOPLO.

Mkuu wa zimamoto mkoa Kagera, Inspekta Hamis Dawa akimvisha cheo askari aliyepandishwa cheo kutoka na tukio la maokozi ya kutoa kwenye shimo la choo mtoto wa mwaka mmoja.

Tukio hilo limefanywa na Mkuu wa jeshi hilo mkoani humo, Inspekta Hamis Dawa kwenye viwanja vya ofisi za Zimamoto mkoa zilizopo Manispaa ya Bukoba ikiwa ni utekekezaji wa tamko la Kamishina Jenerali  wa Jeshi la Zimamoto na Maokozi,  John Masunga.

Inspekta Dawa, amesema sababu ya askari huo, kupandishwa cheo ni kutokana na kitendo alichofanya Mei 21 mwaka huu kuingia kwenye shimo la choo cha Shule ya Msingi Murgwanza na kumuokoa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetupwa na mtu asiyejulikana .

Akizungumzia mazingira na jinsi alivyoweza kukuta mtoto akiwa hai Koplo Minja, amesema ndani ya shimo hilo kulikuwa na miti aina ya mbao ambazo ziliachwa na mafundi ujenzi.

Ameeleza kuwa mbao hizo zinazotumika kusaidia mafundi kuingia na kutoka wakati wa ujenzi ndizo zilisaidia mtoto huyo kunasa kwenye mbao na kushindwa kudumbukia moja kwa moja hadi chini.

"Kwa mazingira niliyoyakuta mule ndani ni kwamba kuna mbao zilizokuwa zinatumiwa na mafundi wakati wa ujenzi ndizo zilimsaidia mtoto hakuweza kushuka moja kwa moja"amesema Koplo Minja

Ameendela kueleza kuwa licha ya mbao baadhi zilikuwa zimeoza  kutoka na hali ya choo ilikuwa zinakatika na kudondoka chini.

Ameongeza kuwa mtoto huyo alikuwa amelala ubavu na kusababisha kupata majeraha mkononi na kuleta madhara ya mguu kwa jinsi na hivyo kuwa akionekana.

Amesema kuwa baada ya kumfikia mtoto huyo alikuta  amefungwa na kanga mdomoni ambayo ilikuwa inamzuia kutoa sauti ya kulia vizuri aliweza kuitoa.

"Nilitoa kanga mdomoni na kutolea uchafu alikuwa nao kwani ile pia inamziba kutoa sauti kulingana na jinsi kanga ilivyokuwa imezungushwa" ameeleza Koplo Minja

Kwa upande wa maelezo ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nyamiyanga,  Daktari William Mnyonyela aliyempokea mtoto huyo amesema baada ya kufanyiwa uchunguzi walibaini kuwa alivinjika mguu wa kushoto na anaendelea kupatiwa matibabu.

Amesema kuwa walifanya taratibu za kumpeleka katika vipimo vya mionzi (X-Ray) katika Hospitali ya Omulugwanza wilayani Ngara kwa uchunguzi zaidi juu ya mwili wake. 

Habari Kubwa