Akizungumza nyumbani kwao Salasala, Dar es Salaam, leo amesema; "Siri ya mafanikio haya ni Mungu, nilikabidhi masomo haya kwa Mungu naye amenisaidia,wazazi wamekuwa msaada mkubwa kwangu pia wamekuwa mfano mzuri sana,mfano mama yangu ni daktari wa falsafa amenihamasisha sana," amesema na kuongeza;
"Pia nilijitahidi kupanga muda wangu vizuri nilihakikisha nina muda wa kusoma,kusali na kufanya mambo muhimu ya shule.Haya ndiyo yalinipa mafanikio haya."
Naye,Mama wa mwanafunzi huyo,Beatrice Halii, amesema wanamshukuru Mungu amewapa kicheko kupitia mtoto wao na kwamba uwezo wake ulijukana akiwa darasa la kwanza na walimuendeleza kwa bidii hadi sasa imedhihirika.
Amewashauri wazazi kitambua karama za watoto na kuzilea,huku akieleza kuwa binti huyo alikuwa akiomba zawadi, basi ni kitabu cha masomo na kwamba anapenda sana kusoma vitabu ili kujiongezea maarifa.