SMZ kushirikiana na wadau kuinua elimu

30Mar 2021
Rahma Suleiman
Zanzibar
Nipashe
SMZ kushirikiana na wadau kuinua elimu

WAZIRI wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar, Simai Mohammed Said, amesema atahakikisha anashirikiana na kila mdau wa elimu ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kupiga hatua kwa kuongeza kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi.

Amesema kumekuepo matatizo mengi kwa walimu hasa waliotumikia muda mrefu kazini na hivyo kusaabisha kupungua kwa ufanisi katika utendaji wa kazi zao.

Ameyasema hayo leo katika mkutano na walimu wenye matatizo ya maradhi mbalimbali pamoja na wanaokaribia kustaafu kazi, kwa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kiembe Samaki.

Amesema atahakisha matatizo yao yatafanyiwa kazi hatua kwa hatua ili kuleta mabadiliko katika maeneo mbalimbali ya sekta hiyo.

Amesema ni changamoto kubwa kwa walimu kupata matatizo ya kiafya na baadhi yao ni kutokana na miundombinu chakavu ilioko katika Shule pamoja na vifaa wanavyofanyia kazi.

Amesema mapinduzi ya kielimu yanahitaji mkazo wa kila mtu, hivyo aliwataka walimu hao kuendelea kuwa na uvumilivu huku matatizo pamoja na madai yao yakiendelea kufanyiwa kazi.

Amesema lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kuhakikisha inaboresha huduma mbalimbali kwa wananchi wake kwa kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora unaimarika zaidi nchini kote.

Habari Kubwa