Spika aelekeza magari ya viongozi kubana mafuta

18May 2022
Romana Mallya
DODOMA
Nipashe
Spika aelekeza magari ya viongozi kubana mafuta

SPIKA wa Bunge, Tulia Ackson, amesema katika kupunguza matumizi ya fedha, magari ya viongozi ambao hawapo kwenye itifaki ya vyombo vyao kuendelea kuunguruma wakiwa wameshuka, yazimwe kwa sababu matumizi kwenye mafuta ni makubwa.

SPIKA wa Bunge, Tulia Ackson.

Aliyasema hayo jana bungeni jijini Dodoma na kueleza kuwa magari ya viongozi ikiwa ni pamoja na ya mawaziri na manaibu waziri yanaendelea kuunguruma nje ya Bunge wakati wao wakiwa bungeni.

"Waheshimiwa wabunge mjue hili na upande wa serikali ninatamani tuone magari ya viongozi yakishashusha kiongozi siyo hapa bungeni tu nchi nzima dereva akishamshusha awe ni Mwenyekiti wa halmashauri, meya, Katibu Mkuu au kiongozi yoyote, ukiacha wale viongozi ambao kwa itifaki yao inabidi magari yaendelee kuwaka, mengine yote inabidi yazimwe na dereva ashuke kwenye gari.

"Ashuke kwa sababu matumizi ya fedha kwenye eneo la mafuta yanakuwa makubwa sana kwa sababu ya magari kuendelea kuwaka wakati kiongozi hayupo kwenye gari, yupo kwenye mkutano wa saa mbili huku gari likiendelea kuwaka.

Kutokana na hilo, Spika Ackson aliomba hilo litazamwe.

"Hili mlitazame na Mheshimiwa Waziri Mkuu uko hapa tunatamani tuone mabadiliko kwenye hili eneo ili matumizi ya serikali yapungue kwenye eneo la mafuta," alisema.

Habari Kubwa