Spika Ndugai aumizwa na tabia ya watu kuwekwa rumande hovyo

04May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Spika Ndugai aumizwa na tabia ya watu kuwekwa rumande hovyo

SPIKA Job Ndugai, ameonyesha kuumizwa na kuwepo kwa tabia ya Polisi kukamata watu hovyo hata wengine ambao wana heshima zao na wanajulikana mahali wanapoishi lakini wanarundikwa tu rumande pasipokuwa na ulazima wowote.

Spika Job Ndugai

"Inatakiwa tujifunze kwa nchi za wengine ambapo mtu huwa anaitwa kituoni na kufanyiwa mahojiano kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kwasababu anafahamika na hawezi kukimbia. Huku ukishakuwa Askari tunaona kuweka watu ndani ni raha"

"Hiki kitu binafsi kinaniuma sana, mtu anawekwa ndani wiki nzima au mwezi halafu baadae anakuja anaachiwa wakati shughuli zake nyingi zimeshasimama. Sheria nazo hata ukitoka huwezi kudai chochote" amesema Ndugai.

 

Habari Kubwa