Ahadi hiyo ilitangazwa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Jasson Rweikiza, wakati wa hafla iliyoandaliwa na shule hiyo kumpongeza kutokana na ushindi wake.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Constansia Buhiya na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Kheri James.

Dk. Rweikiza alisema mbali na kumsomesha bure, shule hiyo itampa Sh. 3,000,000, kumpeleka kumtambulisha bungeni Dodoma yeye na wazazi wake na kubandika picha yake kwenye magari yote 51 ya shule hiyo.
Aliwataka wanafunzi wahitimu kuacha kubweteka huku akiwasisitiza kusoma na kujituma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika kasomo yao na mitihani kwa ujumla.

“Niwashukuru walimu kwani walipambana sana hadi kufanikiwa kupata mafanikio haya, pia nimshukuru mkuu wa shule kwa uongozi bora pamoja na wanafunzi wote waliofanikiwa kufanya vizuri katika mitihani yao na niwasisitize mwendelee kusoma kwa bidii kwani taifa linawategemea,” alisema Rwaikize.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James, alimpongeza mwanafunzi huyo na kumtaka aendelee kufanya vizuri kwenye masomo yake ya sekondari.
Alisema kwa matokeo hayo ni ishara kwamba wazazi na walimu wanatimiza majukumu yao huku akitoa wito kwa wazazi walezi na jamii kuwalea watoto katika maadili mema na kutoa kipaumbele kwenye elimu ili baadaye wajisaidie na kulisaidia taifa kwa ujumla.
“Kwa niaba ya serikali tunampongeza kijana Haule kwa kuwa Tanzania One kwa mwaka huu. Leo Tanzania nzima wanaijadili St. Anne Marie kwasababu ya mtoto huyu, hii ni safari ya kwanza ambayo umeanza tunatarajia utafanya vizuri zaidi katika ngazi zinazoendelea,” alisema James.
Mwisho