Sugu na mwezake wafikishwa mahakamani leo

22Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Sugu na mwezake wafikishwa mahakamani leo

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’  leo Junuari 22. 2018 amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kusikiliza kesi inayomkabili  ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wakiingia mahakamani.

Sugu pamoja  Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga walifikishwa mahakamani hapo Januari 19, 2018 lakini  mahakama ilizuia dhamana zao na kuwarejesha rumande hadi leo.

Siku hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite alitoa uamuzi wa kuwarejesha rumande, kwamba kesi hiyo inatakiwa isikilizwe mfululizo kwa muda mfupi na washtakiwa wakiwa wanafika mahakamani hapo wakitokea mahabusu.

Sugu na mwenzake wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambayo waliyatoa katika mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Habari Kubwa