Sweden yatoa bil.20/- kuendeleza ubunifu

22May 2022
Renatha Msungu
Dodoma
Nipashe Jumapili
Sweden yatoa bil.20/- kuendeleza ubunifu

​​​​​​​SERIKALI ya Sweden kupitia shirika lake la maendeleo (SIDA) limetoa zaidi ya Sh. bilioni 20 kwa ajili ya kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu nchini walioshinda katika mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga, aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya washindi 83 wa mashindano ya ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).Kipanga alisema serikali pia imetenga zaidi ya Sh. milioni 700 kwa ajili ya kuendeleza bunifu za wabunifu walioshinda katika mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyofikia jijini Dodoma.

Alisema fedha hizo zimetolewa na wafadhili hao kwa lengo la kuendeleza ubunifu kwa washindi wa mashindano hayo.

“Tunashukuru wenzetu wa SIDA wametuunga mkono katika mashindano haya, tulikutana nao kuzungumza wakakubali kutuunga mkono ndani ya kipindi cha miaka mitano,”alisema Kipanga.

Akizungumza kuhusiana na fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuendeleza bunifu zilizoshinda, Kipanga alisema fedha hizo zitatumika ipasavyo ili kuhakikisha bunifu zinaendelezwa na kuingizwa sokoni na ziweze kutatua kero zilizopo kwenye jamii.

Alisema hayo ni moja ya maagizo ya Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, aliyeagiza kazi za wabunifu walioshinda kuhakikisha zinaendelezwa na kuingia sokoni ili ziweze kulinufaisha taifa na wabunifu wenyewe.

Alisisitiza kuwa katika Bajeti ya Wizara ya mwaka 2020/23 watawekeza Sh. bilioni tisa kutoka Sh. bilioni tatu ambazo zilitengwa kwa ajili ya wabunifu mwaka 2021/2022.

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk. Amos Nungu, alisema lengola mafunzo hayo kwa wabunifu ni pamoja na kuwajengeauwezo.Alisema wanafanya hivyo ili wabunifu waweze kubadilishana mawazo lakini pia kuangalia namna gani hizi wataziendeleza baada ya mafunzo.

Dk. Nungu alisema katika Sh.milioni 700 ambazo zimetengwakuendeleza ubunifu, Sh. milioni 250 zitatumika kumwendeleza mbunifu wa mita ya maji aliyeshinda mwaka juzi katika mashindano hayo, huku Sh. milioni 500 zitatumika kuendeleza bunifu zilizoshinda mashindano ya mwaka huu.

Habari Kubwa