Taasisi yatoa elimu bure

27Sep 2021
Yasmine Protace
Dar es Salaam
Nipashe
Taasisi yatoa elimu bure

TAASISI ya Mutembei Holding Limited (MHL), inawapatia elimu bure wanafunzi zaidi ya 60 katika shule zake za awali na sekondari.

Kupatiwa elimu kumetokana na wanafunzi hao kutokuwa na wazazi.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Peter Mutembei, katika mahafali ya 18 ya kidato cha nne katika shule ya St. Marks, iliyopo Mbagala jijini Dar es Salaam.

"Taasisj yenu inamiliki shule za sekondary shule St.Mathew's, St.Mark's, Victoty, Imagevosa,Ujenzi na shule ya msingi St. Mathew,s ambapo watoto 64 wanawasomesha bure kutokana na kutokuwa na waza," alisema.

Alisema mbali nakuwasomesha bure watoto hao pia walimu ambao Ni wanyakazi katika shule zao na watoto zao wanasoma nao wanasoma bure katika zao.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, ya St . Mark's Leticia Joseph alisema kuwa ,shule yao imejipanga kimikakati ikiwamo kuwasaidia wanafunzi wasio na uwezo darasani ili nao waweze kuwafikia wenzao. na itawasaidia kujipatia maendeleo.

Alisema kuwa wanawafundisha watoto maadili ili waweze kwendana na tamaduni zinazoendana na mila na tamaduni zote.

Alisema katika masuala ya usalama yapo katika vipengele vinne.

Alivitaja vipengele hivyo kuwa ni usafi,usalama wa afya,akili na uchocheaji wa ukuaji wa mtoto..

Aliongeza kuwa katika mafanikio kutaaluma asilimia kubwa watoto ufaulu.

Alisema mwaka 2020 wanafunzi wa kidato cha nne walifaulu kwa asilimia kwa asilimia 99,huku wa kidato cha pili wakifaulu kwa asilimia 98.

Aliongeza kuwa mkakati mwingine ni kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza mwaka huu wote wanafaulu .

Akizungumza motisha alisema kuwa wanafunzi wanaofanya vizuri upewa motisha ,kwa upande wa wafanyakazi upewa motisha yavyeti na pesa.

Aliongeza kuwa motisha kwa wazazi ni punguzoo la ada linatolewa pale mtoto atakapofanya vizuri mitihani yake.

Pia alipongeza serikali kwa kuwahimiza wananchi kuchukuwa hatua dhidi ya kupambana na Ugonjwa wa korona.
Mgeni rasm katika mahafari hayoShamira Mshagama,ambaye ni mkurugenzi kutoka Taasisi ya Mwanamke na Uongozi,.

Alisema kuwa taasisi yao inahamasisha wanawake katika masuala ya Uongozi.

Alisema wanafunzi wanatakiwa kusoma ili kuyafikia malengo yao.

"Mwanafunzi asipokuwa na msingi mzuri wa elimu hawezi kuyafikia maendeleo aliyokuwa anayataka kuyafanya",alisema.

Pia aliwataka wanafunzi kuwa makini na mitandao ,pale wanapomaliza shule wasijiingize katika matumizi ya mabaya ya mitandao ya jamii

Katika risala ya wahitimu wa kidato cha nne iliyosomwa na Sumaiya Masudi ,risala hiyo ilisema kuwa wanaohitimu wapo 58.

Alisema katika matokeo ya mtihani wa kidato cha pili ufauluulikuwa kwa asilimia 96.

Aliongeza kuwa,katika matokeo ya kujipima na shule za Wilaya ya Temeke wamekuwa wakifanya vizuri.