TAFFA wailalamikia Wakala wa vipimo

28May 2019
Zanura Mollel
NAMANGA
Nipashe
TAFFA wailalamikia Wakala wa vipimo

Chama cha Mawakala wa Forodha mpakani Namanga,Mkoani Arusha,(TAFFA),wamelalamikia hatua ya Wakala wa Vipimo (WMA) kubadilisha mfumo wa ulipaji wa mzigo inayoingia nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa TAFFA, Ismail Kilas, amesema mabadiliko ya ulipaji wa mizigo inayoingia nchini yamebadilika ghafla jambo ambalo litasababisha uchumi wa nchi na wafanyabiashara kuporomoka.

Ameeleza kuwa, hapo awali walikua wakilipia thamani ya mzigo kwa asilimia 0.2 ambayo sheria inawaongozakufanya hivyo, kama mzigo upo chini ya Shilingi 100,000 katika upande wa thamani mteja analazimika kulipia kiasi hicho hicho. 

"Hapo awali walikua wakilipa kwa thamani ya mzigo ukiingia nchini lakini kwa sasa wakala wa vipimo wamewaletea mabadiliko ya kulipia kwa kila mzigo, ambapo kama gari moja ikibeba mizigo 30 wanalazimika kulipia kila 'iteam' shillingi 100,000" Amesema Kilas

Amedai kuwa hakuna kifungu cha sheria kinacho waongoza WMA kutoza fedha kwa kila mzigo mmoja mmoja uliopo kwenye gari, bali sheria inasema kila gari ilipie 0.2 ya thamani ya mzigo waliobeba.

Hata hivyo alieleza kuwa mabadiliko hayo yanaelekea kukwamisha shughuli za kibiashara katika mpaka wa Namanga, Sirarali na Mtukulu ambako sheria hiyo imeanza kutumika huku katika mipaka mingine iliyopo nchini kutokumika kwa sheria hiyo. 

Amelaani kitendo cha serikali kuketi na kupitisha sheria hizo bila kuwashirikisha wadau au watumiaji wa sheria hiyo ambao kwa sasa inaonekana kuwa kandamizi kwao.

Aidha chama hicho kimeweka msimamo Wa pamoja na kudai kuwa hawapo tayari kuendelea kufanya kazi na wakala Wa vipimo,huku wakidai fedha za mizigo ambayo haistahili kulipiwa walizolipia kwa muda mrefu kuzihitaji kwani wakala hao walizilipisha kimakosa

"Kuna mizigo ambayo haistahili kuchajiwa mfano malighafi ya kupeleka kiwandani kwa ajili ya kuzalisha bidhaa zingine lakini hapa wapo mawakala wamelipia hizo malighafi,fedha hizo tunazipate,tunaomba Waziri mkuu aingilie kati jambo hili" amedai Kilas

Ameongezea kuwa magari yamepaki kwa zaidi ya siku tano mpakani hapo kutokana na Mabadiliko ya ulipiaji katika kitengo cha Vipimo ,kutokana na mvutano uliokua ukiendelea baina yao na mawakala Wa vipimo

" Tumepokea barua inayotutaka kulipia kwa iteam,lakini sheria haizungumzi hivyo,ndiyo maana tumegoma kuvusha mizigo ,japo kuna wasaliti waliovusha lakini hao ni wale wenye iteam 1 hadi 3 lakini mtu mwenye iteam 80 ni vigumu ,Ukipiga mahesabu ya pesa tunayoilipa kwa iteam inazidi thamani ya manunuzi ya mizigo " alieleza Ismail

Mkurugenzi wa ufundi WMA, Stela Kahwa akiwa katika Ofisi zilizopo mpakani Namanga (OSBP).

Naye Mkurugenzi wa ufundi kitengo cha vipimo (WMA) Stela Kahwa amesema kuwa ameyapokea malalamiko hayo na anayafanyia kazi ili kuweza kubaini ukweli Wa jambo hilo.

"Nimepokea malalamiko haya,nayafanyia kazi lakini nimeelekeza itumike sheria ya awali ya malipo kwa ya mzigo  Kwa FOB na siyo kwa iteam" amesema Kahwa

Habari Kubwa