TAG yampa tuzo Magufuli mapambano dhidi ya corona

14Aug 2020
Na Mwandishi Wetu
DODOMA
Nipashe
TAG yampa tuzo Magufuli mapambano dhidi ya corona

Baraza Kuu la Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), limemkabidhi Tuzo maalum Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli kwa kutambua mchango wake katika kuliongoza Taifa kumtegemea Mungu katika kipindi cha janga la Virusi vya corona nchini.

Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dk. Barnabas Mtokambali akimkabidhi Rais Magufuli tuzo ya mapambanio ya corona.

Tuzo hiyo amekabidhiwa leo Agosti 14, 2020 na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dk. Barnabas Mtokambali, katika Mkutano Mkuu wa 13 wa Baraza kuu la Kanisa la TAG, wakati akifungua mkutano huo uliofanyika Dodoma.

Aidha Askofu Mtokambali amesema kuwa jambo lililofanywa na Rais Magufuli katika kipindi kile la kuruhusu shughuli za kimaendeleo ziendelee kama kawaida, lilikuwa la tofauti kwani ni katika kipindi hiko ambapo Mataifa mengine yaliweka nguvu yakuzuia watu wasitoke majumbani.

 

Habari Kubwa