Tahadhari uwepo upepo mkali mikoa mitano, Zanzibar yatolewa

23Aug 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Tahadhari uwepo upepo mkali mikoa mitano, Zanzibar yatolewa

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya kuwepo upepo mkali na mawimbi makubwa katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa ya utabiri wa hali ya hewa iliyotolewa na TMA, inaonyesha kutakuwa na upepo mkali sambamba na mawimbi makubwa kwa siku tano yaani kuanzia Agosti 21 hadi 25.

Mikoa hiyo ni Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Angalizo hilo la upepo mkali limetolewa pia kwa baadhi ya maeneo ya Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.

Mamlaka hiyo imewataka watumiaji wa bahari na maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari.

Tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa imetolewa kwa maeneo ya ukanda wa pwani yote, katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kulingana na taarifa hiyo, athari zinazoweza kutokea ni matatizo ya usafiri, kuhatarisha maisha kutokana na uwezekano wa boti/meli kuzama, kutawanyishwa/kupeperushwa kwa takataka, kuathirika kwa shughuli za uvuvi na ucheleweshwaji wa usafiri baharini.

Imeandikwa na Adelina Charles, TUDARCo

Habari Kubwa