Tahadhari mvua kubwa mikoa 7

11Jan 2020
Elizaberth Zaya
Dar es Salaam
Nipashe
Tahadhari mvua kubwa mikoa 7

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya kuwapo kwa siku mbili za mvua kubwa kwenye mikoa saba kuanzia jana.

Mikoa itakayopata mvua hiyo kwa mujibu wa TMA ni Singida, Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Dodoma.

Meneja wa Utabiri kutoka Kituo Kikuu cha Utabiri TMA, Samuel Mbuya, aliwataka wakazi wa mikoa hiyo kuchukua tahadhari.

"Ni vyema watu wakachukua tahadhari ikiwamo kuzibua mifereji ili kuruhusu maji yasituame sehemu moja, maana hiyo ndiyo chanzo cha mafuriko, lakini pia kuhakikisha wanawahi kwenda kwenye maeneo yao ya kazi na kuondoa msongamano barabarani," alishauri.

Kwa mujibu wa meneja huyo, mamlaka itaendelea kutoa tahadhari, angalizo na taarifa mbalimbali za hali ya hewa kwa wananchi, ili kuwakinga na majanga yanayoweza kutokea kwenye jamii.

Habari Kubwa