"TAKUKURU wachunguze mradi bwawa la maji Maratani"- Aweso

29Jul 2021
Na Mwandishi Wetu
NANYUMBU - MTWARA
Nipashe
"TAKUKURU wachunguze mradi bwawa la maji Maratani"- Aweso

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza TAKUKURU kuchunguza utekelezaji wa Bwawa la kuhifadhia maji la Maratani lililopo wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara ambalo limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.139. 

Watumishi waliotakiwa kufika TAKUKURU ni Peter Mdalangwila (Meneja wa RUWASA Uchimbaji-DDCA) na Mhandisi Renard Baseki (Aliyekuwa Meneja wa RUWASA Wilaya ya Nanyumbu aliyehamishiwa Wilaya ya Newala).

Lengo la agizo hilo la Aweso alilolitoa leo ni kubaini thamani ya fedha iliyotumika na hali halisi aliojionea ambayo hairidhishi baada ya kufika katika eneo hilo.

Katika eneo hilo, Waziri Aweso amepokelewa na umati wa wananchi wanaoishi eneo la bwawa hilo waliokuwa wakimsubiri kutoa malalamiko yao kutokana na changamoto kubwa ya maji inayowakabili.

Utekelezaji wa Ujenzi wa bwawa hilo umefanywa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)kupitia Idara ya Uchimbaji-DDCA.