TAKUKURU yachunguza na kukamilisha kesi 1079

28Mar 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe Jumapili
TAKUKURU yachunguza na kukamilisha kesi 1079

​​​​​​​MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Brigedia Jenerali John Mbungo, amesema katika ripoti ya mwaka 2019/2020 taasisi hiyo imechunguza na kukamilisha jumla ya kesi 1079.

“Taasisi ilichunguza na kukamilisha majalada 1079 yenye tuhuma mbalimbali ikiwemo ukwepaji kodi, matumizi yasiyo sahihi ya manunuzi ya umma, vyama vya ushirika wa masoko ya mazao kutowalipa wakulima, mikopo umiza na ufujaji fedha kwenye miradi ya maendeleo,” amesema Mbungo.

Amesema kati ya majalada hayo, majalada 385 yalihusu hongo, majalada 694 yalihusu vifungu vingine vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Brigedia Mbungo amesema majalada 443 yaliwasilishwa katika Ofisi ya Taifa ya mashtaka kuombewa vibali kuwafikisha watuhumiwa mahakamani na kesi mpya ni 586.

“Kesi mpya 381 na kati yake zilizotolewa uamuzi na 267 walikutwa na hatia na kuhukumiwa vifungo au kulipa faini zikiwemo kesi tatu kutoka mahakama kuu ambazo zilihusishwa na mahakama ya mafisadi na zipo kesi nne zenye hadhi ya mahakama za mafisadi zinazoendelea mahakamani, “ amesema Mbungo

Habari Kubwa