Takukuru yamshikilia aliyekuwa bosi MSD

02Jun 2020
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
Takukuru yamshikilia aliyekuwa bosi MSD

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamshikilia aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Madawa nchini (MSD), Laurian Bwanakunu, kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara.

Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Madawa nchini (MSD) Laurian Bwanakunu.

Katika taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyoiliyotolewa kwa vyombo vya habari  imeeleza kuwa pamoja na aliyekuwa Mtendaji mkuu huyo inamshikilia pia Kaimu Mkurugenzi Lojistiki wa bohari hiyo ya madawa Byekwaso Tabura.

“Pamoja na mtendaji mkuu huyo yupo kaimu mkurugenzi wa lojistiki wa MSD Byekaswo Tabura ambao wote kwa pamoja wapo mahabusu katika ofisi za Takukuru Upanga Jijini Dar es Salaam ili kupisha uchunguzi “ inasema sehemu ya barua hiyo.

Habari Kubwa