Takukuru kuwabana wakopeshaji riba kubwa mtaani

09Apr 2020
Enock Charles
Dar es Salaam
Nipashe
Takukuru kuwabana wakopeshaji riba kubwa mtaani

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Brigedia John Mbungo amesema taasisi hiyo itaendelea kupambana na wakopeshaji wa mitaani ambao wamekuwa wakiwabambikiza watumishi hasa walimu riba kubwa kupita kiasi na ambazo kisheria hazikubaliki.

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Brigedia John Mbungo.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Aprili 9,2020 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi huyo amesema taasisi hiyo haitakivumilia kikundi chochote chenye mikopo inayowaumiza wananchi na kwamba watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Uchunguzi wa Takukuru waathirika wakubwa wa uwepo wa kikundi hiki ni wastaafu na hususan waalimu” amesema Brigedia Mbungo.

Amesema katika rekodi ya kesi ambazo wanazifahamu ni mstaafu mmoja aliyekopa Sh. 900,000 ili alipe Sh 1,260,000 kwa riba ya asilimia 40 ambayo bado iko juu lakini alilazimika kulipa Sh. milioni 12,500,000 malipo haya ni sawa na riba ya asilimia 300. 

Amesema mstaafu mwingine alikopa Sh. milioni 5 ili alipe Sh.  milioni 7 sawa na kwa riba ya asilimia 40 lakini badala yake alilipa Sh. milioni 20 sawa na riba ya asilimia 300.

Amesema kwa Mkoa wa Mara pekee hadi kufikia Aprili 2020 tayari taasisi hiyo ilifanikiwa kuwarejeshea wastaafu fedha walizokuwa wameporwa kiasi cha shilingi 289,000,000 pamoja na nyumba ya mjane yenye thamani ya shilingi milioni 40.

Ameeleza urejeshaji wa fedha uliofanyika kupitia opesheni iliyofanywa na taasisi hiyo kwa vikundi hivyo katika mikoa mbalimbali alisema Mara sh.289,000,000 na nyumba moja ya thamani y ash.milioni 40,Tabora Sh.41,200,00 ,Katavi 29,000,000 Mwanza 17,440,375 Kagera 10,000,000 Njombe Sh.5,000,000 huku Rukwa wakimkamata mkopeshaji mwenye kadi 85 za benki.

Habari Kubwa