Takukuru Longido yaonya rushwa uchaguzi mdogo

12Oct 2019
Zanura Mollel
Longido
Nipashe
Takukuru Longido yaonya rushwa uchaguzi mdogo

KAMANDA wa TAKUKURU Wilaya ya Longido mkoani Arusha Ally Mikidadi amewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na kuwataka kutoa taarifa za watangaza nia wanao toa rushwa ili wapate nafasi za uongozi.

KAMANDA wa TAKUKURU Wilaya ya Longido mkoani Arusha Ally Mikidadi.

Kauli hiyo ameitoa leo Oktoba 12,2019 wakati akizungmza na Nipashe ofisini kwake na kueleza kuwa ni kosa la jina kutoa ,kupokea au kushawishi rushwa chini ya kifungu 15 na 11/2007.

Amesema kuwa kutoa rushwa au kupokea pia ni kinyume na sheria ya Serikali za mitaa sura ya 287 na sheria za serikali za miji sura ya 288 juu ya chaguzi za serikali za mitaa mwaka 2019.

" Kumchagua kiongozi anayetoa rushwa ni kukwamisha maendeleo ya nchi,chagueni viongozi watakao leta maendeleo,watoa rushwa wananunua madaraka,mkiwapa nafasi watakuja kuwahujuhumu warejeshe fedha zao walizotumia kipindi cha kampeni.," Amesema Mikidadi

Habari Kubwa