TAKUKURU yamdaka mkufunzi chuo cha kilimo rushwa ya ngono

08Apr 2021
Lilian Lugakingira
BUKOBA
Nipashe
TAKUKURU yamdaka mkufunzi chuo cha kilimo rushwa ya ngono

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, John Joseph, amesema wanamshikilia Ruta Kyaragaine (59) mkufunzi wa Chuo cha Kilimo Maruku, Bukoba, kwa tuhuma za kumuomba rushwa ya ngono mwanachuo wa kike ambaye jina lake limehifadhiwa, ili amsaidie kufaulu mitihani yake.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera John Joseph.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera John Joseph amesema kuwa mtuhumiwa huyo Ruta Kyaragaine (59) amekuwa akimtisha mwanachuo huyo kuwa asipomkubalia atasababisha ashindwe kufaulu mitihani.

"Kufuatia kupokelewa kwa taarifa hiyo, tulianza kufanya uchunguzi na tarehe 03/04/2021 tulimkamata mkufunzi huyo akiwa katika nyumba ya kulala wageni iliyoko katika Manispaa ya Bukoba jina linahifadhiwa, akiwa na mwanachuo huyo" amesema Joseph.

Habari Kubwa