Takukuru yamnasa mkuu wa shule akiomba rushwa ya ngono

15Dec 2019
Renatha Msungu
Dodoma
Nipashe
Takukuru yamnasa mkuu wa shule akiomba rushwa ya ngono

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoani Dodoma imefanikiwa kumkamata mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Serengeti iliopo mkoani Mara Baraka Sabi (41)-

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo.

-akiomba rushwa ya ngono kwa Mwanafunzi  wa kike aliyehitimu kidato cha sita Katika shule hivyo mwaka 2016 ili ampatie cheti chake cha kuhitimu. 

Mwanafunzi  huyo ambaye jina lake linahifadhiwa kutokana na usalama wake alikuwa anahitaji cheti chake kwa ajili ya kwenda kufanya tartibu za kuomba ajira baada chuo kikuu UDSM. 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kuhusiana na sakata hilo. 

Kibwengo amesema baada ya Binti huyo kuwasiliana na mwalimu mkuu huyo alimtaka waonane jijini Dodoma ambako alikuwa anahudhiria mkutano wa wakuu wa shule jijini hapa. 

Kibwengo amesema Mwanafunzi huyo ambaye hivi sasa ni muhitimu wa chuo kikuu UDSM baada ya kuona Mwalimu huyo amemwambia asubiri cheti atakuja nacho yeye ndipo akaamua kwenda kutoa taarifa Takukuru kuhusiana na rushwa ya ngono. 

" Mwalimu huyo alimwambia mwanafunzi aende Pai hoteli iliopo jijini hapa Ili ampatie cheti hiko na alipofika alimwambia waende katika chumba walichofikia na kumwambia ampe rushwa ya ngono ndio atampa cheti chake, "amesema Kibwengo. 

"Mwanafunzi baada ya kuona hivyo alimwambia Mwalimu Baraka kuwa wafanye tendo hilo kesho kwa sababu siku hiyo hakuwa vizuri, "amesema Kibwengo. 

Amesema siku inayofuata Mwanafunzi huyo alitekeleza sharti la kwenda kujamiana ndipo Takukuru walifanikiwa kumkamata kumkamata mwalimu mkuu huyo na kuhakikisha ili taratibu za kisheria zifuatwe. 

Kibwengo amesema mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo kinyume na sheria kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 ya  marejeo 2018.

Amefafanua zaidi ya kuwa kosa hilo ni la jinai na mwanafunzi ameona umuhimu wa kuvunja ukimya kuhusiana na vitendo hivyo. 

Hata hivyo amesema Takukuru ilifanikiwa kupata cheti cha mtoa taarifa na kuongeza uchunguzi wa suala hili unaendelea ili taratibu za kisheria na hatua stahiki zitachukuliwa. 

Aidha Takukuru imeomba wananchi kuendelea kushirikiana na wadau ili kuendeleza kampeni ya vunja ukimya kataa rushwa ya ngono ili kuhamasisha wananchi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa ya ngono. 

Habari Kubwa