Ofisa hiyo ambaye ameshafukuzwa kazi tangu Julai 30, mwaka huu, aliomba na kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabishara wawili waliokuwa akiwachunguzwa kwa makosa mbalimbali yakiwamo ya ukwepaji kodi.
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Diwani Athumani, aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa, ofisa huyo alipewa jukumu la kuwachunguza watuhumiwa hao Februari mwaka huu na badala yake aliwaomba rushwa.
"Napenda kutamka tena mbele ya umma kwamba muda wowote nikiwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, sitakuwa tayari kumvumilia mtumishi yoyote awe ni wa Takukuru au nje ya Takukuru ambaye atajihusisha na vitendo vya rushwa," Athumani alisema.