Akitoa taarifa ya utekelezaji kwa waandishi wa habari jana, Mkuu wa TAKUKURU mkoani hapa, Dk. Damas Sutta, alisema walifanikiwa kurejesha fedha na nyumba hizo baada ya kupokea malalamiko na kuyafanyia kazi.
Alisema kiasi hicho cha fedha kiliokolewa kutoka kwa kampuni, watu binafsi, pamoja na watumishi wa umma ambao hufanya kazi zao bila kuzingatia sheria na kanuni za nchi.
Alitaja sehemu ya fedha zilizookolewa kuwa ni za kampuni ya kuuza mbegu, Highland Seeds ya jijini Mbeya, Sh. 4,491,600 kutoka kwa wananchi waliokopa mbegu.
Alisema fedha nyingine zilizookolewa ni Sh. 1,200,000 ambazo mkazi wa Mtaa wa Ilembo, wilayani Mbozi, Emiliana Sakimela, alimkopea Kaimu Ofisa Mtendaji wa Mtaa Ilolo, Rehema Mwandulusya, kutoka kwa watu mbalimbali na kugoma kurejesha.
Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com