Tamisemi watakiwa kuchukua tahadhari kidato cha sita wakirjea shuleni

22May 2020
Augusta Njoji
Dodoma
Nipashe
Tamisemi watakiwa kuchukua tahadhari kidato cha sita wakirjea shuleni

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), anayeshughulikia Elimu, Mwita Waitara ameagiza viongozi wa Mikoa, Wilaya na uongozi wa shule za kidato cha sita kuchukua tahadhari zote za afya ikiwemo wanafunzi wa bweni kulala kwa umbali ili kujiepusha na ....

maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Tahadhari zingine ni kuhakikisha wanafunzi na walimu wanavaa barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka kwenye maeneo yote ya kuingilia shuleni na madarasani.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Waitara amesema kabla ya shule hizo kufunguliwa Juni Mosi viongozi hao wakague na kuhakikisha mazingira rafiki yanakuwepo.

"Kuna uwezekano wazazi wakaingia gharama kidogo maana wanapaswa kuwanunulia barakoa, lakini na watakaoweza kuwanunulia  vitakasa mikono ili kujikinga na ugonjwa wa Corona," amesema.

Amesema walimu waandae wanafunzi kisaikolojia ili wafanye vizuri kwenye mitihani yao.

"Wanafunzi wanaweza kwenda na tangawizi na hata kujifukiza pia ruksa na wanafunzi wote lazima wapimwe joto," amesema.

Amesisitiza kuwa wanafunzi wanapaswa kuripoti shule kwa muda uliopangwa na kutakuwa na adhabu za utoro kwa ambao hawataripoti kwa wakati.

Habari Kubwa