TAMISEMI yaomba bajeti ya Sh 7.68 trilioni

19Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
TAMISEMI yaomba bajeti ya Sh 7.68 trilioni

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imeliomba Bunge kuwaidhinishia Sh 7.68 trilioni kwa ajili ya mwaka wa fedha 2021/22.

Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu ameomba kiasi hicho leo, Aprili 19 alipowasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake.

Amesema kati ya fedha hizo Sh 4.72 trilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh2.95 trilioni ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo Sh1.67 trilioni zitakuwa fedha za ndani na Sh1.27 trilioni zitatoka nje.

"Mwaka ujao wa fedha serikali itajenga hospitali mpya 28 katika halmashauri ambazo hazina hospitali za serikali kwa gharama ya Sh. bilioni 14,"

"Mwaka ujao wa fedha 2021/22 Serikali itafanya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya hospitali 31 za awamu ya pili kwa gharama ya Sh.bilioni 12.30 ambazo ni fedha za ndani," amesema.

"Serikali inatarajia kujenga nyumba za walimu 300 kea gharama ya Sh. Milioni 50 kwa kila nyumba".

Habari Kubwa