TANAPA yahamasisha utalii wa ndani vyuo vikuu

15Jan 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
TANAPA yahamasisha utalii wa ndani vyuo vikuu

Shirika la Hifadhi za Taifa  Tanzania ( TANAPA) kupitia Kanda ya Magharibi leo  limefanya  Kongamano la Wanazuoni wa Vyuo Vikuu na Kati vilivyopo ndani ya Mkoa wa Mwanza.

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahifadhi wa hifadhi za kanda ya ziwa.

Kongamano hilo lililenga kuhamasisha Viongozi wa Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuanza kushiriki kikamilifu katika uhamasishaji wa Utalii wa Ndani katika Jamii zilizopo katika Vyuo Vikuu nchini.

Aidha, Kongamano hilo lililokuwa na Kauli Mbiu ya ni zamu ya Wasomi Twendezetu Kutalii  limetegua kitendawili cha kwanini  wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Kati ndani ya Mkoa wa Mwanza hawajahamasika kutembelea vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya Kanda ya Ziwa. 

"Kongamano hili limekuwa na mafanikio makubwa ambapo jumla ya viongozi wa Serikali za Wanafunzi 100 na wakufunzi 30 kutoka katika jumla ya vyuo vikuu na vya kati 27 wameshiriki,"Alisema Kamishana Msaidizi Uhifadhi-Mawasiliano wa TANAPA, Pascal Shelutete 

Aidha, alisema mikakati mbalimbali ya kuhamasisha utalii wa Ndani Ndani ya Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa imewekwa lengo ni kuongeza idadi ya watalii wa ndani.

Habari Kubwa