Gari hilo lenye namba za usajili T 917 BCN lilipakia pamba hiyo ikiwa imekusanywa nyumbani kwa mtu katika kata ya Gilya Wilayani Bariadi kinyume na utaratibu kwani utaratibu umeelezwa kuwa pamba yote inatakiwa kununuliwa kupitia vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS)
Akizungumza katika eneo la tukio leo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga aliagiza gari hilo pamoja na Dereva kushirikiwa na jeshi polisi mpaka pale wanunuzi wa pamba hivyo watakaposakwa na kupatikana mara moja.
"Ninaliagiza jeshi la polisi kuendelea kulishikiria gari hilo pamoja na dereva huku wakiwasaka wanunuzi wa pamba hiyo watafutwe ili waje kujibu kosa hilo la kununua na kusafirisha kimagendo ,pia nawasihi wanunuzi hao wajitokeze Mara moja na kujisalimisha wenyewe," amesema Kiswaga
Aidha Dereva wa gari hilo Lulyalya Deus hiyo alieleza kutowafahamu wanunuzi wa pamba hiyo kwani yeye alilipwa malipo ya kazi ya kuisafirisha na kukiri kushuhudia pamba hiyo kuanzia inapopakiwa kwenye gari na kwamba alikiri watu hao walimlipwa walitoroka pale ambapo gari lilisimamishwa kwa ajili ya ukaguzi.
Hata hivyo katika kukabiliana na wizi wa pamba Wilaya humo, Mkuu wa wilaya amewataka watendaji wa mitaa na kata kuwa walinzi katika maeneo yao na kuhakikisha hakuna pamba inayonunuliwa bila kufuata utaratibu.