TANROADS yatakiwa kuwakata fedha wakandarasi wanaochelewesha kazi

06Aug 2022
Mary Geofrey
MWANGA
Nipashe
TANROADS yatakiwa kuwakata fedha wakandarasi wanaochelewesha kazi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuwakata fedha wakandarasi wanaochelewesha miradi ili kujenga nidhani ya uwajibikaji.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, leo ametembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwanga - Kikweni Vuchama na kuongea na wananchi wa Vuchama Ngofi kata ya Mwaniko, wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ametoa agizo hilo, wakati akikagua barabara ya Mwanga, Kikweni hadi Vuchama yenye urefu wa Kilometa 29 inayoendelea kujengwa na kuagiza mkandarasi kukatwa fedha kutokana na kuchelewesha kazi hiyo.

Chongolo yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siu tano ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, miradi ya maendeleo na kuhimiza ushiriki wa sensa ya watu na makazi.

Ameagiza fedha aatakazokatwa mkandarasi anayejenga barabara hiyo, zitumike kuongeza ujenzi wa kipande kingine ili kuendelea kukamilisha kazi inayoendelea.

Awali Meneja wa TANROADS mkoa wa Kilimanjaro, Motta Kyando, alisema ujenzi huo umegharimu Sh.milioni 960 na lengo la mradi huo ni kukamilika Agosti 8,mwaka huu lakini bado kazi kubwa haijafanyika.Mwisho

Habari Kubwa