Tanzania kutuma wataalamu wa madini Botswana

10Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Tanzania kutuma wataalamu wa madini Botswana

Tanzania inakusudia kutuma timu ya wataalamu nchini Botswana kwa ajili ya kujifunza namna bora ya kusimamia rasilimali ya madini.

Hayo yamesemwa leo Juni 10, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, na rais Samia Suluhu Hassan, wakati wa ziara ya siku mbili ya rais wa Botswana Dk. Mokgweetsi Masisi yenye lengo la kuimarisha ushiriakiano kati ya Tanzania na nchi hiyo pamoja na uwekezaji.

Samia amesema kuwa Botswana ni moja ya nchi zinazouza kiwango kikubwa cha madini ya almasi duniani.

"Ziara yako nchini inatoa fursa ya kukuza uhusiano na urafiki wa kihistoria kati ya mataifa yetu mawili, kama mnavyofahamu Tanzania na Botswana ni nchi marafiki na uhusiano wetu ulianza tangu enzi za harakati za ukombozi," amesema.

Aidha rais Samia amesema kuwa biashara kati ya Tanzania na Botswana imeongezeka kutoka Mil 731/- kwa mwaka 2005 hadi kufikia Bil 3.5 kwa mwaka huu.

"Biashara kati ya Tanzania na Botswana imeongezeka kutoka shilingi za Tanzania Mil.731 mwaka 2005 hadi kufikia shilingi Bil. 3.5 mwaka 2021. Botswana imewekeza nchini katika miradi yenye thamani ya USD Mil. 231 na kutoa ajira 2128 kwa Watanzania," amesema Samia.

Habari Kubwa