Tanzania ya 9 uwazi wa manunuzi ya umma duniani

21May 2019
Salome Kitomari
DAR
Nipashe
Tanzania ya 9 uwazi wa manunuzi ya umma duniani

TANZANIA imeshika nafasi ya tisa kwenye uwazi wa mikataba ya manunuzi ya umma kati ya nchi 25 duniani.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika Lisilo la Kiserikali la Maendeleo Hivos, imeonyesha kuwa katika eneo la uwepo wa sheria zinazosaidia utekelezaji wa manunuzi ni asilimia 1

Ripoti hiyo imeonyesha kuwa kwenye ufanisi wa manunuzi ya umma Tanzania imepata asilimia 90.

Aidha, kwenye eneo la uwajibikaji Tanzania imepata asilimia 71.43, huku kwenye eneo la ushindani imepata asilimia 89.5.

Ripoti hiyo imeonyesha kuwa Tanzania haijafanya vizuri kwenye eneo la uwazi kwenye utaratibu wa manunuzi ya umma kwa kupata asilimia 34.4.

Aidha, ripoti hiyo imebainisha kuwa mfumo wa kushughulikia manunuzi kielektroniki umesaidia kuwezesha utaratibu wa manunuzi kufanyika kirahisi.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa mifumo iliyojengwa kwenye utaratibu wa manunuzi, ikiwamo kutangaza zabuni na kuwezesha wahusika kuzijaza kirahisi zaidi.

Aidha, kwenye eneo la kutoa zabuni Tanzania imepata asilimia 80.

Habari Kubwa