Tanzania Yamchagua Dk. Magufuli Tena

31Oct 2020
Na Mwandishi Wetu
UCHAGUZI 2020
Nipashe
Tanzania Yamchagua Dk. Magufuli Tena
  • Rais mteule anatarajiwa kuhutubia nchi kesho Jumapili Oktoba 1 2020

Tanzania imemchagua tena rais aliyeko madarakani John Pombe Magufuli kushika ofisi ya urais kwa miaka mingine mitano.

Rais Magufuli ameshinda uchaguzi 2020 kwa kishindo kikubwa akiwa amepata zaidi ya kura milionni kumi na mbili kutoka kwa wapiga kura zaidi ya milioni ishirini.

Rais Dk. John Pombe Magufuli achaguliwa kuiongoza Tanzania kwa muhula mwingi wa miaka mitano.

Tanzania imemchagua tena rais aliyeko madarakani John Pombe Magufuli kushika ofisi ya urais kwa miaka mingine mitano.

Rais Magufuli ameshinda uchaguzi 2020 kwa kishindo kikubwa akiwa amepata zaidi ya kura milionni kumi na mbili kutoka kwa wapiga kura zaidi ya milioni ishirini.

Ushindi wake umeambatana na wimbi kubwa la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikichukua ngome nyingi za upinzani.

Baadhi ya ngome za upinzani lilizo kwenda CCM ni pamoja na majimbo ya Arusha Mjini, Hai, Kilimanjaro, Mbeya Mjini, Kigoma na Kawe Dar es Salaam.

Vivyo hivyo Chama Cha Mapinduzi kimeshinda urais visiwani baada ya Zanzibar kumchagua Dk Hussein Ali Mwinyi  kwa asilimia 76 .

Uchaguzi huu ni wa sita wa nchi tangu uchaguzi wa vyama vingi uanze tena mwanzoni mwaka 1992. Mwaka 1995 Tanzania ilifanya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi ambapo rais wa marehemu Benjamin Mkapa alichaguliwa kuingia madarakani na kushika madaraka kwa miaka kumi.

Mwaka 2005 Tanzania ilifanya uchaguzi wa pili wa vyama vingi ambapo rais Jakaya Kikwete alichukua madaraka na kutawala kwa muongo mmoja.

Mnamo mwaka 2015, rais Dkt Magufuli alichukua madaraka na baada ya kushinda uchaguzi huu, amekuwa ni rais wa 3 wa CCM kutawala nchi kwa vipindi viwili chini ya uongozi wa vyama vingi.

Rais mteule atapokea cheti cha urais Jumapili hii ya Oktoba 1 2020 ambapo anatarajiwa kuhutubia nchi. Usipitwe, kwa habari na uchambuzi wa kina bofya hapa: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa