Tanzania yamuunga mkono Ramaphosa

04Sep 2019
Romana Mallya
Dar es Salaam
Nipashe
Tanzania yamuunga mkono Ramaphosa

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema serikali ya Tanzania inamuunga mkono Rais wa Afrika Kusini,  Cyril Ramaphosa kwa jitihada alizozianzisha kuhusiana na vurugu zilizotokea nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi.

Prof. Kabudi amesema serikali ya Tanzania imeridhishwa na matamshi na tamko la Rais huyo ambalo limekuwa wazi kwamba hali hiyo siyo nzuri.

"Wananchi wa Afrika Kusini ambao wamepitia kipindi cha madhira ya ubaguzi wa rangi tunawasihi waelewe kwamba adui wao siyo waafrika wenzao, ni wakati wa kukaa chini na wao wakatafakari, wakaelewa kwamba hali waliyonayo haikuchangiwa na haichangiwi na waafrika wenzao bali mfumo wa uchumi ambao awali ulijengwa katika misingi ya ubaguzi wa rangi na uliwafanya wengi wakose uhuru wao.

"Mpaka sasa hakuna taarifa za mtanzania yeyote kuuwawa, na kuhusu kuvunjiwa maduka bado tunafuatilia," amesema Prof. Kabudi

Prof. Kabudi amewahakilishia raia wa Afrika Kusini waliopo Tanzania kuwa, wataendelea kuwa salama wao na mali zao.

"Kuhusu vurugu zilizotokea nchini humo kama Tanzania hatujafikia hatua ya kuwarejesha nchini watanzania waliopo huko,"  amesema.

Habari Kubwa