Tanzania yaongoza kwa mchele safi

14Mar 2018
Na Mwandishi Wetu
MOSHI
Nipashe
Tanzania yaongoza kwa mchele safi

TANZANIA imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazozalisha mpunga mzuri na msafi ambao una thamani zaidi ya unaozalishwa nchini Msumbiji, Kenya, Rwanda na Burundi.

Aidha, imetajwa kuwa nchi yenye idadi kubwa ya wanawake wanaozalisha kwa wingi zao hilo, tani tano hadi nane kwa hekta ikilinganisha na nchi ya Msumbiji na Kenya.

Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa kilimo kutoka Jimbo la Zambezia, nchini Msumbiji, Jaime Gado, alipotembelea nchini akiwa na timu ya wataalamu wa  mpunga saba na mtaalamu mmoja kutoka nchini Japan, kwa lengo la kubadilishana ujuzi na kujifunza kutoka kwa wakulima wa Tanzania kuhusu namna ya kuzalisha mpunga bora.

Gado alisema mbali na changamoto ya kuwa na mashine zilizochakaa na ubovu wa miundombinu ikiwamo barabara, bado mkulima wa Tanzania amekua na ari ya kuzalisha mpunga ulio bora.

"Tumeona changamoto kadha wa kadha, lakini bado mkulima huyu amekua akizalisha kilicho bora, tatizo ni uhakika wa soko, naishauri mamlaka husika kuangalia namna ya kumsaidia mkulima huyu, ili pia aweze kuuza kwa wingi katika nchi zinazozunguka Bara la Afrika," alisema.

 

Habari Kubwa