Tasaf yaweka kambi Longido

24Jun 2019
Zanura Mollel
LONGIDO
Nipashe
Tasaf yaweka kambi Longido

TASAF Makao makuu imewezesha mafunzo ya awali ya vikundi vya kuweka na kukuza uchumi wa kaya masikini katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha  iliziweze kujitegemea hata pale mradi huo utakapo fikia kikomo.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo.

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Mifugo, Nestory Dagharo amesema Halmashauri hiyo inawalengwa 5,641 wanao nufaika na mradi wa kusaidia kaya masikini. 

Ameeleza kuwa wilaya hiyo ina vijiji 49 lakini hadi sasa ni vijiji 27 ndio vilivyopo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini huku wanawake wanao nufaika na fedha hizo jumla ni 3,296 na wanaume wakiwa 227.

Dagharo amedai kuwa Halmashauri hiyo inajumla ya vikundi 249 vinavyo nufaika na miradi mbali mbali ya Tasaf na vimepiga hatua katika nafasi ya kuweka na kukopa fedha ili waweze kujikimu mahitaji yao ya kifamilia.

"Wamefikia hatua ya kuweka million 56 na hata sasa million 34 zimetolewa kama mkopo hii ni hatua nzuri mliofanikiwa kupata mafunzo haya nendeni mkawasaidie ambao hawajapata na hata vile vikundi ambavyo havipo kwenye mpango wa Tasaf hii ni fursa kwao" Amesema Dagharo

 Mkuu wa Idara ya mawasiliano anayeshughulikia malalamiko kutoka Makao Makuu Tasaf Makwinja Dismass, ameeleza kuwa ili kaya ziweze kujikwamua katika nafasi za umasikini ni wajibu wawe na mikakati ya ruzuku ya msingi na yenye masharti pamoja na  kuwatengenezea ajira za muda.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Nestory Dagharo akizungumza na walengwa wa mafunzo hayo.

Amesema lengo hasa la kuwezesha mafunzo haya ni kuhakikisha kaya hizo zinafikia hatua za kujimudu zenyewe katika nafasi ya Elimu kwa watoto,matibabu ya afya kwa kutumia bima na kuhakikisha lishe bora inapatikana kwa Siku Milo mitatu.

"Mafunzo haya ni ya siku tano katika Wilaya hii lakini tumetenga Siku ya alhamis na ijumaa kutembelea vijiji vilivyopo katika mpango huu kuona namna wanavyo endesha miradi yao " alisema Dismass

Mkuu wa idara ya mawasiliano anayeshughulikia changamoto kutoka Makao makuu Tasaf ,Makwinja Dismass.

Alifafanua kuwa kuwepo kwa vikundi vya ufugaji kuku,Ng'ombe ,mbuzi na kondoo pamoja na kilimo cha mbogamboga kutawasaidia walengwa hawa kutanua uchumi wao ,hivyo ni muhimu kuwapa Elimu namna watakavyoweza kuziendesha miradi waliyoibuni .

Estomi Paul mwezeshaji kutoka Halmashauri ya Longido alieleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni matumizi ya lugha pamoja na walengwa wa miradi  ya Tasaf kuto hudhuria vikao maalumu mara nyingi wao hupenda vikao vyenye malipo ya fedha za Tasaf.

Mratibu wa Tasaf Wilaya ya Longido, Lobulu Saruni.

" Tunaenda vijijini tunaitisha vikao lakini hawatokei,ila ukitangaza vikao vya kupokea fedha hakuna anayekosa kufika pia lugha ya vijijini ni lugha mama ya kimaasai nayo ni changamoto sana" alidai Estomi

Naye Mratibu Wa Tasaf wilayani hapa Lobulu Saruni alidai kuwa mafunzo haya ni mwendelezo Wa shughuli zinazotekelezwa na Tasaf ndani ya Longido katika viji 22 ndani ya kaya 18 zenye tarafa nne.

Habari Kubwa