TASAF yatoa mafunzo uhakiki wa walengwa wa kaya masikini   

04Aug 2020
Hamisi Nasiri
Masasi
Nipashe
TASAF yatoa mafunzo uhakiki wa walengwa wa kaya masikini   

 JUMLA ya wawezeshaji 86 wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) ngazi ya halmashauri,kutoka wilaya ya Masasi mkoani Mtwara  wamepatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya kufanya zoezi la uhakiki wa walengwa wa kaya masikini ili kuondoa kaya zote ambazo zimepoteza sifa za kuwepo kwenye mpango huo.

Wawezeshaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wakiwa katika mafunzo maalum.

Mafunzo hayo yaliyofanyika siku mbili  wilayani Masasi mkoani Mtwara yalitolewa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) makao makuu ambapo washiriki  86 wamepata fursa  ya kushiriki mafunzo hayo kwa nadharia na vitendo .

 Akifungua mafunzo hayo Mwakilishi wa Tasaf kutoka makao makuu, Josephine Joseph alisema kuwa lengo kuu la Tasaf kutoa mafunzo  kwa wawezeshaji hao ni kuwapatia uelewa kabla ya kuwafikia walengwa katika jamii na kutekeleza zoezi hilo la uhakiki.

   “Mafunzo haya yanayofanyika hapa leo yanalenga kujenga uelewa wa pamoja wa namna zoezi hili la uhakiki wa walengwa litakavyofanyika na kwamba zoezi hili litabaini kaya zote ambazo zimepoteza sifa ya kuwepo katika mpango na zitaondolewa,”amesema Joseph 

 Amesema ili kupata orodha halisi ya walengwa kwenye masjala ya kaya za walengwa lakini pia kufahamu walengwa ambao wamefariki.

Habari Kubwa