Taulo za kike kutatua changamoto utoro wanafunzi Tabora

15Aug 2019
Na Waandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Taulo za kike kutatua changamoto utoro wanafunzi Tabora
  • *Ni kupitia kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na East Africa Television na East Africa Radio

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amefichua siri kuwa chanzo cha utoro wa wanafunzi katika mkoa wake hususani wa kike ulichangiwa na uwezo duni wa wanafunzi hao kushindwa kununua taulo za kike wanapopata hedhi na kupelekea kutoudhuria masomo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Aggrey Mwanri akiongoza zoezi la utoaji wa taulo za kike katika shule ya Sekondari Ndono, iloyopo Wilayani Uyui kupitia kampeni ya Namthamini. Kushoto kwa mkuu wa mkoa ni Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Isaya Msuya.

Kauli hiyo ameitoa wakati akipokea taulo za kike kutoka www.eatv.com kupitia Kampeni yake ya Namthamni. 

Amesema kuwa wakati mkoa wa Tabora ulipokuwa ukitajwa kama kinara wa utoro wa wanafunzi chanzo kikubwa kilikuwa ni ukosefu wa taulo za kike kwa baadhi ya wanafunzi wa kike na kupelekea kukaa nyumbani mpaka kipindi cha hedhi kikome.

"Ile kampeni ya "Chikichi" ilianzia hapo walikuwa wanakwenda wale mabinti ukija kucheki sana sana kinachomfanya asikae shuleni kule ni kwamba akiwa katika kipindi kile anaona sasa asubiri mpaka kipindi chote kiishe akisharudi katika hali yake ya kawaida ndio arudi shuleni kule kakutana na fataki kamsomba moja kwa moja," amesema Mwanri

Ameongeza kuwa  walipo anzisha kampneni ya kuhakikisha wanafunzi wanapata taulo za kike mashuleni ilisaidia ikienda sambamba na ushauri kwa vijana ili wasione ni kitu cha ajabu kwa sababu hiyo ni hali ya kawaida kwa wasichana wanaokua. 

" Kwahiyo mimi niliposikia kuwa mnatoa taulo za kike mnakuja hapa niliona inanisaidia kutatua tatizo la msingi kwa wanafunzi wa kike katika Mkoa wa Tabora," amesema Mwanri 

Imeandikwa na Juster Prudence na Adelina Charles, TUDARCO

Habari Kubwa