TB Joshua afariki dunia

06Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
TB Joshua afariki dunia

MHUBIRI wa Kimataifa kutoka nchini Nigeria, Temitope Balogun Joshua maarufu  TB Joshua amefariki dunia jana Jumamosi Juni 5, 2021 nchini  humo.

Temitope Balogun Joshua maarufu  TB Joshua.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kanisa lake la Scoan inaeleza, TB Joshua alifariki muda mfupi baada ya kutoa huduma katika kanisa hilo Jumamosi.

"Jumamosi Nabii TB Joshua alizungumza katika mkutano wa washirika kupitia Emmanuel TV alisema 'kila jambo na wakati wake, kuna wakati wa kuja hapa kwa maombi na wakati wa kurudi nyumbani baada ya ibada'."

"Mungu amemuita nyumbani Nabii TB Joshua kwa mapenzi yake. Nyakati zake za mwisho hapa duniani alizitumia katika huduma ya Mungu. Hiki ndio kitu alichozaliwa kukifanya, alikiishi na kukifia," inaeleza taarifa hiyo.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2014, TB Joshua aliingia kwenye msukosuko baada ya kanisa lake kuporomoka na kuua watu na wengine kujeruhiwa.

Habari Kubwa