TCB yatoa msaada saruji mifuko 100 kukamilisha ujenzi shule ya Itaga

10Oct 2021
Halima Ikunji
Tabora
Nipashe Jumapili
TCB yatoa msaada saruji mifuko 100 kukamilisha ujenzi shule ya Itaga

​​​​​​​BENKI ya Taifa ya Biashara TCB mkoani Tabora imetoa msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa shule ya seminari ya Itaga na kanisa katoliki Ipuli kwa ajili ya kufanikisha ukarabati iliyoghalimu kiasi cha shilingi milioni mbili.

Akitoa msaada huo Meneja wa Tawi la Benki hiyo mkoani hapa Timony Joseph, amesema benki hiyo imeamua kutoa msaada wa mifuko 100 ya saruji katika shule na kanisa ikiwa ni moja ya kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani katika suala zima la elimu.

Meneja huyo amesema pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali lakini shule hiyo ni wadau wakubwa wa kuweka fedha zao katika benki ya TCB hivyo saruji waliyoitoa itasaidia kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo.

Amesema miundimbinu ya shule inapokuwa mizuri inasaidia kwa wanafunzi kusoma masomo yao vizuri ikiwa pamoja na kuongeza vipaji vya elimu.

Akizungumza Jana mara baada ya kupokea mifuko 50 ya saruji mkuu wa seminari ya Itaga, Gombera Padre Joseph Buhili alisema anaishuru benki hiyo TCB kwa kuamua kutoa saruji hiyo ambayo ni tendo la kiungwana sana kuweza kujali na kuona umuhimu wa elimu.

Padri huyo amesema kwamba wameupokea msaada huo kwa mikono miwili na utatumika kwa ajili ya kukarabati majengo ya shule hiyo kwa ajili ya kuwezesha watoto kusoma sehemu salama.

Aidha, amesema kupatika kwa saruji hiyo kutasaidia na wadau wengine kuamua kujitokeza na kutoa msaada kama huo kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule hiyo ambapo mwakani inatimiza miaka 100.

Mifuko ya Saluji iliyotolewa Kanisani na shule ya Seminali ya Itaga Mkoani Tabora.

Amesema shule ya Itaga seminari inajumla ya wanafunzi 230 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita ambao wanafunzi masomo ya kiroho na kimwili ili baada ya kumaliza masomo yao wakalitumikie Taifa na jamii kwa ujumla.

Naye paroko wa Parokia ya Ipuli Padre Ponciano Kibobera ameishukuru bank hiyo kwa kujali na kuona kanisa nalo linapaswa kupata hisani kwa kutoa mifuko ya saruji 50 yenye thamani ya shilingi milioni 1.

Amesema kwamba kanisa hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuingia waumini 4000 kwa wakati moja.

Habari Kubwa