TECNO watoa msaada, elimu kituo cha watoto yatima 

30Jun 2020
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
TECNO watoa msaada, elimu kituo cha watoto yatima 

Kampuni ya simu ya Tecno Tanzania kwa kushirikiana na Startimes Tanzania wametembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Chanika Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwapa misaada mbalimbali pamoja na kutoa elimu ya masuala ya kiafya pamoja na
kuwapatia vifaa vya kujikinga na corona.

Kampuni hiyo pia imetoa elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi hao pamoja na masuala ya kifedha kupitia mwanasaikolojia Antony Luvanda pamoja na shirika lisilo la kiserikali la 'Her Initiative'.

Taarifa iliyotolewa kwa umma inasema kuwa pamoja na hayo pia TECNO imetoa vifaa vya kujikinga na maambukizo ya ugonjwa wa corona kwa wafanyakazi wa kituo hicho kwa lengo la kujikinga wao pamoja na watoto wanaowahidumia katika kituo hicho.

"Washirika wetu Startimes Tanzania wamedhamiria kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapa kingamuzi kipya chenye kifurushi cha mwaka mzima kitakachoonyesha channel zinazotoa mafundisho kwa ajili ya watoto. Shirika la Her Initiative' linategemewa kuwapa elimu ya afya, kujitambua pamoja na ujasiriamali"

"Tunapenda sana kuwashukuru washirika wetu wote waliokubali kushirikiana nasi katika siku hii muhimu sana kwa kampuni yetu inayojali jamii yetu pendwa inayotuzunguka. Pia ningependa kutoa wito na mualiko kwa ninyi ndugu waandishi wa habari kuambatana nasi siku hiyo ya jumamosi maana tunatambua umuhimu wenu katika ujenzi wa taifa haswa kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi."

Habari Kubwa