TIC kushughulikia tatizo la kukatika umeme viwandani

18Apr 2021
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe Jumapili
TIC kushughulikia tatizo la kukatika umeme viwandani

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kimeahidi kushughulikia tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara, ambalo husababisha viwanda kushindwa kufanya uzalishaji wa bidhaa zao kwa ufanisi, huku wakiingia hasara ya kuharibika kwa mitambo.

Meneja wa kituo hicho cha uwekezaji kutoka Kanda ya Ziwa, Pendo Gondwe, amebainisha hayo Leo wakati alipoenda kutembelea kiwanda cha Jambo Food Product kilichopo mkoani Shinyanga, ambacho kina zalisha bidhaa mbalimbali vikiwamo vinywaji.

Meneja kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Pendo Gondwe.

Amesema mara baada ya kufanya ziara fupi ya kutembelea kiwanda hicho na kuona uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, wamepokea changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara ambayo huathiri shughuli zao, na kuahidi kwenda kulifanyia kazi kwa kuzungumza na mamlaka husika.

"TIC tumefanya ziara kwenye kiwanda hiko cha jambo, lengo kubwa ni kuona Shughuli za uzalishaji zinavyo endeshwa na wawekezaji wetu, pamoja na kutatua changamoto ambazo zinawakabili ili wasikwame na kuendelea kuchangia pato la Taifa,"

"Kiwanda hiki pia kimetoa ajiri nyingi kwa wananchi, na kimesaidia kukuza sekta nyingine ikiwamo ya kilimo ambapo kimefunga mashine ya kuchakata matunda, mfano maembe, nanasi,machungwa, na wanatengeneza asali, na malighafi zote hizi hununua kwa wananchi na kukuza uchumi wao," amesema Gondwe. 

Habari Kubwa