TIC yasajili miradi 905 ya uwekezaji ndani ya miaka mitatu

05Dec 2018
Romana Mallya
DAR ES SALAAM
Nipashe
TIC yasajili miradi 905 ya uwekezaji ndani ya miaka mitatu

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa muda wa kipindi cha miaka mitatu kimefanikiwa kusajili miradi 905 kwa wazawa na wawekezaji kutoka nje yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 13.2.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe.

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe, ameyasema hayo leo wakati akizungumzia mafanikio ya miaka mitatu tangu Rais John Magufuli aingie madarakani.

Amesema miradi hiyo ambayo ipo ya kuanzia miaka mitatu hadi mitano itatoa ajira za moja kwa moja 115,055 kwa watanzania.

Mwambe amesema kuwa mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa uwekezaji mkubwa ambapo hadi sasa kwa kipindi cha miaka mitatu umefanyika kwa asilimia 56.9. 

Habari Kubwa