TMDA kutoa majibu athari za P2 hivi karibuni

09Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
TMDA kutoa majibu athari za P2 hivi karibuni

​​​​​​​MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Adam Fimbo, amesema mamlaka hiyo inaendelea kuzifanyia tathimini dawa za kuzuia mimba za dharura (Emergence Contraceptive Pills') maarufu kama P2 ambapo hivi karibuni wataalamu wa afya walisema kuwa vinasababisha madhara kwa-

- watumiaji.

Fimbo amesema hayo katika mafunzo ya wakaguzi wapya kutoka katika Kanda nane, pia amesema kuna taarifa za uwepo wa matumizi holela ya dawa hizo na watakapokamilisha uchunguzi wataweka wazi.

"Kwa sasa tunafuatilia juu ya matumizi yasiyo sahihi kwa kuzifanyia tathimini ya kina kufahamu kwa nini isitumike inavyopaswa”

"Tunafahamu dawa hizi utumiwa endapo umepewa cheti na Daktari ueze kuitumia kwa inavyotakiwa kama inavyikusudiwa hivyo tutakapokamilisha kubaini ukweli wa kwa nini inatumika isivyofaa tutawataarifu.” amesema Fimbo.

Habari Kubwa