TMDA yatoa onyo kwa wavuta sigara, ugoro na tumbaku

20May 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
TMDA yatoa onyo kwa wavuta sigara, ugoro na tumbaku

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TMDA) imesema watu milioni 8 kwa mwaka hufariki kutokana na kansa zinazosababishwa na uvutaji wa sigara huku watu milioni 1.2 wanaokaa karibu na wavuta sigara kupata madhara bili ya wao kujijua.

Akizungumza Mkoani Mtwara, Meneja wa TMDA Kanda ya Kusini Dk. Engelbert Mbekenga amesema kwa mujibu wa tafiti za Shirika la Afya Duniani (WHO) takribani Watu Milioni 8 Duniani wanakufa kutokana na Kansa zinazosababishwa na uvutaji wa sigara na 80% ya vifo hivyo vinapatikana katika Nchi zenye uchumi wa chini huku Tanzania nayo ikiwa ni mingoni.

"Watu milioni 1.2 wamepata madhara bila wenyewe kujua kwasababu ya kukaa jirani na wavuta sigara na wakati wenyewe hawavuti, kuna umuhimu wa kutoa taarifa kwa wale wanaotaka kuvuta wavute eneo lililojitenga na wengine ili wasiotumia wasipate madhara"

"Kuna madhara makubwa yanayotokana na uvutaji wa sigara ikiwemo Kansa inayoshamnulia eneo la upumuaji, kubadilika kwa meno kuwa machafu wakati wote na msongo wa mawazo" amesema Meneja huyo.

Aidha, Mamlaka hiyo imetoa onyo kwa watumiaji wote wa sigara, ugoro pamoja na tumbgaku kutokana na athari za kiafua zinazoweza kuwapata.

Habari Kubwa