TPA,TRA na TRC zachangia ucheleweshaji mizigo bandarini

13Mar 2019
Beatrice Shayo
DAR ES SALAAM
Nipashe
TPA,TRA na TRC zachangia ucheleweshaji mizigo bandarini

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamweli, amesema haridhishwi na operesheni za bandari kwa kuwa kuna taasisi tatu ambazo zinachangia ucheleweshaji wa mizigo ya ndani na nje ya nchi.

bandari ya dar es salaam.

Taasisi hizo ni Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Kamwele aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa utiaji saini makubaliano ya ushirikiano katika ya Shirika la reli Tanzania (TRC) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kukarabati mabehewa 40 ambayo yatagharimu Dola za Kimarekani 600,000 sawa na Sh bilion 1.13.

Habari Kubwa