Tufuatane ukanionyeshe hivyo visima vilipo –Mbunge Maganga

14Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Tufuatane ukanionyeshe hivyo visima vilipo –Mbunge Maganga

MBUNGE wa Mbogwe, Nicodemus Maganga, amemtaka Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, kutofuata mambo ya kwenye makaratasi na kufuatana naye ili akamuoneshe visima 26 ambavyo amesema vipo.

MBUNGE wa Mbogwe, Nicodemus Maganga.

Mbunge huyo amesema hayo leo April 14 Bungeni jijini Dodoma baada ya kuonesha kutoridhishwa na majibu ja Naibu Waziri alilohoji kuwa “Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria katika Jimbo la Mbogwe kwa ajili ya matumizi ya Wananchi”?Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Mahundi amesema hali ya upatikanaji maji ni wastani wa asilimia 55 na huduma inapatikana kupitia miradi minne ya skimu, visima virefu 26, visima vifupi 460 na matenki 50 ya kuvuna maji ya mvua

Baada ya majibu hayo ya Naibu Waziri, Maganga alimtaka kuongozana nae hadi jimboni kwake akamuonyeshe sehemu ambapo visima hivyo vipo."Tuongozane naye akanionyeshe pale vilipo. Mimi ni Mbunge wa Mbogwe na ninaishi Mbogwe, kuna tabu sana katika sekta ya maji" ameongeza Maganga

Habari Kubwa