Tulia Trust yamsafirisha kijana Amos kutibiwa India

03Mar 2019
Frank Monyo
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Tulia Trust yamsafirisha kijana Amos kutibiwa India

Hatimaye kijana Amos Gabriel aliyegharamiwa matibabu na Taasisi ya Tulia Trust usiku wa kuamkia leo ameanza safari ya kwenda kupatiwa matibabu katika Hospitali Neurogen ya nchini India.

Kijana amos Gabriel akiwa na wazazi wake katika uwanja wa ndege wa Dar es salaam tayari kwa safari ya matibabu kuelekea India.

Kijana huyo na mzazi wake wameondoka alfajiri ya Machi 3 ikiwa taratibu zote za matibabu zimeshafanyika pamoja na gharama Hospitali hiyo zimeshalipwa tayari.

Taasisi ya Tulia Trust na wadau mbalimbali wameweza kufanikisha sh. milioni 33 kwa matibabu ya kijana huyo.

Hivi karibuni wakati akikabidhiwa hundi ya sh.milioni 33 kwa mzazi wa Amos, Mwanzilishi wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge Dkt.Tulia A Mwansasu alisema kuwa wanamuombea Mungu aweze kurejea katika hali yake ya kawaida na muendelea na masomo.

Alisema kuwa waliguswa baada ya kuona taarifa katika vyombo vya habari juu madhila yanayomkuta kijana huyo na kwamba kijana huyo ana ndoto ya shule hivyo isiweze kukatishwa.

Mzazi wa Amos amesema anamshukuru Naibu Spika kwa kijitoa na watanzania katika kufanikisha gharama ya matibabu ya kwenda kutibiwa nchini India.

Gabriel anatatizo la uti wa mgongo uliotokana na kuanguka katika mti wakati akikata fimbo ya mwalimu kwa ajili ya kuwachapia wanafunzi.

Habari Kubwa