-mkoani Mtwara.
Dk. Stergomena amesema hayo leo Mei 19, 2022 akiwa Bungeni, ambapo amesema kuwa kundi hilo limekuwa likiathiri usalama kwa kuharibu na kupora mali za wananchi.
"Kundi hilo limekuwa likiathiri usalama kwa kuharibu na kupora mali za Wananchi, katika kupambana na changamoto hii, JWTZ imeendelea kuimarisha ulinzi kwa kufanya operesheni za ndani ya nchi na kukabiliana na kundi hilo"
"Aidha, JWTZ inashiriki operesheni chini ya Mwamvuli wa SADC nchini Msumbiji katika jitihada za kudhibiti ugaidi, operesheni hizi zimeendelea kuimarisha ulinzi katika eneo la Mpaka, kudumisha amani na utulivu, operesheni zimesaidia kupunguza nguvu ya kundi hilo la kigaidi"
"Hata hivyo, kundi hilo linatekeleza mashambulizi kwa kuhamahama na kubadili mbinu za kimapigano licha ya hali hiyo, vikundi vyetu vinaendelea kupambana kuhakikisha kundi hilo halileti madhara zaidi" amesema Dk. Stergomena.