Tunahitaji Katiba Mpya kulinda haki za kisiasa, kiuchumi na kiraia

13May 2022
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Tunahitaji Katiba Mpya kulinda haki za kisiasa, kiuchumi na kiraia

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo,  Ado Shaibu ameweka bayana kuwa pamoja na mambo mengine,  chama hicho kinataka Katiba Mpya ili kuweka misingi imara ya kulinda haki za kisiasa na kiraia.

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu.

Ado ameyasema hayo leo akitoa salamu za Vyama vya Siasa kwenye Maadhimisho ya Miaka 10 ya Jukwaa la Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa PSSSF, Dar es salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

"Ni kweli uwanja wa kisiasa (political space) na kiraia (civic space) umeanza kufunguka. Leo hii, THRDC wasingeweza kufanya shughuli kama hii miaka michache iliyopita kwa sababu Akaunti zao za Benki zilifungiwa. Kwa hili, tunampongeza Mh. Rais"

"Hata hivyo, ACT Wazalendo hatutaki suala hili liendelee kuwa hisani ya Mh. Rais. Tunataka Katiba Mpya ili iweke misingi madhubuti ya kisheria kulinda haki za kisiasa, kiuchumi na kiraia"- amesema Ado na kuongeza kuwa;

"ACT Wazalendo tunataka Mchakato wa Katiba Mpya uanze sasa sambamba na mchakato wa Tume Huru ya Uchaguzi. Watetezi wa Haki za Binadamu tunapaswa kuungana kwenye hili" amesema 

Habari Kubwa