Tunamshikilia Sheikh Ponda kwa mahojiano- Mambosasa

12Jul 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Tunamshikilia Sheikh Ponda kwa mahojiano- Mambosasa

JESHI la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa ponda, kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na  uchochezi walioutoa kwenye waraka juu ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Sheikh Issa ponda.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo.

“Tunaye sisi Polisi, tumemkamata kwa mahojiano ya uchochezi walioutoa kwenye kitu walichokiita waraka, hivyo tunamhoji kutokana na ule waraka” Mambosasa

Aidha, Kamanda Mambosasa amesema licha ya viongozi wote wa Taasisi ya Sheikh huyo kuukana kupitia vituo mbalimbali vya radio na runinga lakini Shekh ponda amekukubali kuwa waraka huo wake pamoja na taasisi yake.

Habari Kubwa