Ubunge CUF hadharani Julai 17

14Jul 2020
Elizaberth Zaya
Dar es Salaam
Nipashe
Ubunge CUF hadharani Julai 17

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema kinatarajia kuhitimisha kazi ya kura ya maoni kwa nafasi ya wagombea ubunge, Julai 17.

Akizungumza na Nipashe jana, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF Taifa, Juma Kilaghai, alisema wameshaanza mchakato huo.

“Tumeshaanza mchakato wa kura ya maoni kwa wagombea wa nafasi za ubunge na kwa baadhi ya mikoa tumeshamaliza, ni maeneo machache tu ambayo yamebaki ambayo mpaka kufikia Julai 17 tutakuwa tumemaliza, ”alisema Kilaghai.

Pia, alisema kwa upande wa madiwani wameshamaliza kazi hiyo ya kura za maoni.

“Kwa madiwani tayari tumemaliza, tuna uhakika tutasimamisha madiwani zaidi ya asilimia 80 nchi nzima,” alisema Kilaghai.

Habari Kubwa